Wakulima wagawiwa mbegu Kwale

Martin Mwanje
1 Min Read
Gavana Fatuma Achani wakati wa kuwagawia wakulima mbegu

Serikali ya kaunti ya Kwale imezindua zoezi la ugavi wa tani arobaini na tano za mbegu kwa wakulima wa kaunti hiyo.

Mpango wa kuwagawia wakulima mbegu hizo umezinduliwa katika wadi zote 20 za kaunti ya Kwale.

Gavana Fatuma Achani akizindua zoezi hilo katika makao makuu ya kaunti ya Kwale, amewarai wakulima kutumia fursa hii ya msimu wa mvua ndefu kupanda mbegu mashambani ili kukabiliana na janga la njaa katika siku za usoni.

Achani amesema kuwa mbegu hizo za bila malipo kwa wakulima zitawasaidia kupata mavuno ya kutosha na kukabiliana na ukosefu wa chakula katika jamii.

“Kama serikali, tunapanga kuwapa wakulima wetu vifaa muhimu vya upanzi wakati tukiukaribisha msimu uliosubiriwa wa mvua za kipindi kirefu,” alisema Gavana huyo.

Mbegu hizo ni pamoja na mahindi, pojo, kunde na mpunga.

Aidha, wakazi wa Kwale wamehimizwa kupanda miche wakati wa msimu huu wa mvua.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa kaunti hiyo Roman Shera alipongeza juhudi za utawala wa Gavana Achani na kutoa wito kwa wakulima kutumia vilivyo mbegu hizo kuongeza uzalishaji.

Pongezi sawia zilitolewa na Mercy Chalika, mkulima katika kaunti hiyo.

“Nawatia moyo wakulima wenzangu kujinufaisha na msaada wa kilimo unaotolewa na serikali,2 alisema Chalika.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *