Joto la kisiasa linazidi kupanda katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, DRC, zikisalia takriban siku 34 kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu.
Hali ya ukosefu wa usalama imeanza kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo nchini humo na kusababisha hofu kuu.
Viongozi wa shirikika la maendeleo kusini mwa Afrika, SADC wanatarajiwa kukutana mjini Luanda, Angola kujadili maswala kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa usalama nchini DRC.
Awali, SADC ilikubali kutuma wanajeshi 500 kudumisha usalama nchini DRC, lakini bado hatua hiyo haijatatua hali ya ukosefu wa usalama kutokana na ongezeko la makundi haramu kila kuchao.
Rais Felix Tshisekedi anakabaliana na wapinzani wengine 20 katika harakati za kuwania kuhifadhi kiti chake kwa muhula mwingine ingawa idadi hiyo huenda ikapungua tarehe 18 mwezi huu, wakati makahama ya kikatiba ikapowatathmini kubaini ufaafu wao.
Wagombeaji wengine wa kiti cha urasi wameelezea hofu yao kuhusu uwazi wa uchaguzi huo mkuu wakisema serikali imepanga njama ya kuiba kura.