Wakenya zaidi wanaendelea kurejeshwa hapa nchini kutoka Thailand, huku kundi lingine likitarajiwa kuwasili Jumamosi alasiri.
Kundi la asasi mbalimbali likiongozwa na katibu wa maswala ya Ughaibuni Roseline Njogu, litawapokea wakenya hao katika Uwanja wa Ddege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) saa sita na nusu adhuhuri.
“Katibu Roseline K. Njogu, na maafisa wengine kutoka kundi la asasi mbalimbali, wakenya hao,” ilisema taarifa kutoka kwa idara ya maswala ya ughaibuni.
Kurejea kwa wakenya hao, kunafuatia kuwasili hapa nchini kwa Wakenya 48, walionusiriwa na serikali kutoka nchini Myanmar.
Katika miaka ya hivi karibuni, mamia ya wakenya wamejipata katika kile iinachoaminika kuwa ulanguzi wa binadamu baada ya kuhadaiwa kwamba wanaenda kupata kazi nzuri nchini Thailand.
Maafisa kutoka Thailand, China na Myanmar mnamo mwezi Februari mwaka huu, walisambaratisha vituo vya ulanguzi wa binadamu katika mpaka wa Thailand na Myanmar, na kuwaachilia huru maelfu ya raia wa kigeni.