Wakenya wawinda dhahabu 3 Budapest katika siku ya mwisho ya mashindano ya Riadha ya Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha wa Kenya watajitosa uwanjani katika fainali tatu katika siku ya mwisho ya makala ya 19 ya mashindano ya Riadha Duniani  Jumapili usiku mjini Budapest nchini Hungary.

Fainali ya kwanza kwa Wakenya itakuwa mita 5,000 wanaume kuanzia saa tatu na dakika 20 usiku,Jacon Krop aliyeshinda nishani ya fedha mwaka uliopita akishirikiana na Ishmael Kipkurui.

Upinzani kwa Wakenya utatoka kwa mshindi wa nishani ya fedha mwaka uliopita nchini Marekani Oscar Chelimo aliyeshinda medali ya shaba mwaka 2022 na Waethioipia Berihu Aregawi,Hagos GEBRHIWET na Yomif Kejelcha pamoja na Yakub Ingebrigsten wa Norway.

Fainali ya pili kwa wanariaha wa Kenya itakuwa mita 800 kwa vipusa kuanzia saa nne kasorobo usiku bingwa wa Jumuiya ya madola Mary Moraa atakayekabiliana na bingwa mtetezi Athing Mu wa Marekani,Keely Hodgson wa Uingereza pamoja na Halimah Nakaayi wa Uganda.

Beatrice Chepkoech anayeshikilia rekodi ya dunia ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji atawaongoza bingwa wa Jumuiya ya Madola Jackline Chepkoech na bingwa wa dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Faith Cherotich fainali ikianza saa nne na dakika tano usiku.

Kenya ni saba kwenye msimamo wa medali kwa dhahabu 2 fedha 2 na shaba 2.

Share This Article