Uwanja wa kaunti ya Kwale unatarajwia kuboreshwa baada ya Gavana Fatuma Achani kupokea vifaa kutoka kwa Wizara ya Michezo kutimiza ahadi ya Rais William Ruto wakati wa sherehe za mwaka jana za Siku ya Mashujaa.
Gavana Achani akizungumza baada ya kupokea viti 8,000 na milingoti ya lango la uwanja wa soka, amempongeza Rais Ruto kwa ukarimu huo akiongeza kuwa utasaidia kaunti hiyo kuafikia viwango vinavyohitajika vya michezo.
Uwanja wa Kwale unaselehi mashabiki 13,000, na msaada huo wa vifaa utasaidia kuafikia viwango vya kimataifa.