Wakenya watalenga kufunga mashindano ya Riadha Duniani kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, kwa ushindi siku ya Jumapili mjini Oregon,Marekani.
Jumla ya wanariadha sita wa Kenya watakuwa uwanjani katika fainali tatu.
Fainali zitakazowashirikisha Wakenya ni pamoja na mita 1500 kwa wanaume ambapo Wilson Chepkwech watashirikiana na bingwa wa afrika David Kapaiko.
Aidha, bingwa wa Afrika Caren Chepchirchir atajitosa uwanjani kwenye fainali ya mita 1500 pamoja na Josephine Sembeyo.
Baada ya kutwaa pia ubingwa wa Afrika,Emmanuel Someki atashirikiana na Nicholas Losiwareng kwenye fainali ya mita 3,000 kuruka maji na viunzi.
Kenya imenyakua nishani 2 za dhahabu,fedha moja na shaba 2 kufikia sasa.