Vinara wa Ligi kuu Uingereza,Arsenal, walijikatia tiketi kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 20.
Washika bunduki Arsenal, waliwahi tiketi ya fainali baada ya kuwatema nje Atletico Madrid, bao moja bila jibu katika marudio ya nusu fainali Jumanne usiku kiwarani Emirates.
Vijana Wa Mikel Arteta, walifuzu kwa fainali Kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1,baada ya mkumbo wa kwanza kumalizikia sare ya bao moja jijini Madrid, wiki Jana.
Masmm
Mashabiki Wa Arsenal wakisherehekea kufuzu fainali
Arsenal wanasubiri mshindi kati ya Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, na mabingwa wa Ufaransa, PSG, watakaopambana leo katika nusu fainali ya pili.
PSG wanaongoza mabao 5-4, kutokana na duru ya Kwanza.
Fainali itasakatwa Budapest nchini Hungary Mei 30.