Wakenya wahimizwa kulinda na kudumisha utamaduni

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua akiwa katika kaunti ya Kajiado.

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa wakenya kudumisha mila na utamaduni, ili kuimarisha uthabiti na umoja wa taifa hili.

Akizungumza leo Jumamosi katika kaunti ya Kajiado, naibu huyo wa Rais alisema yuko katika mstari wa mbele kukuza utamaduni za jamii hapa nchini.

“Lazima tufurahie utamaduni wetu. Mimi ni mtetezi mkuu wa utamadfuni wetu, na ipo haja ya kuulinda ili kuimarisha taifa letu,” alisema Gachagua.

Aliyasema hayo alipohudhuria makala ya 25 ya maombi ya muungano wa madhehebu mbalimbali ya jamii ya Kimaasai, katika uwanja wa shule ya msingi ya Inkinyie kaunti ya Kajiado.

Gachagua alipongeza jamii ya Maa kwa kulinda utamaduni wake hapa nchini na pia katika ngazi za kimataifa.

“Jamii ya Maa, inafahamika kote duniani kutokana na utamaduni wake wa kipekee,” alidokeza Gachagua.

Wakati huo huo, Gachagua alipongeza juhudu za maafisa husika za kukabiliana na matumizi ya pombe haramu na mihadarati.

Alisema vita dhidi ya mihadarati vinaendelea ili kuhakikisha uovu huo unatokomezwa.

Website |  + posts
Share This Article