Wakenya sita wauawa nchini Somalia

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakenya sita wameuawa mjini Dhobley nchini Somalia katika shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kundi la Al Shabaab.

Hii ni kwa mujibu wa Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Liboi Ali Manduku.

Manduku amesema kuwa sita hao ni wa kutoka eneo la Meru nchini Kenya na walikuwa wakichuuza vyombo vya plastiki mjini Dhobley.

Hata hivyo, haijulikani ni vipi Wakenya hao walijipata nchini Somalia, licha ya mpaka wa Kenya na Somalia kufungwa.

Share This Article