Wakazi wa Kisumu wapongeza ufadhili mpya wa SGR

Tom Mathinji
1 Min Read
Reli ya kisasa ya SGR

Wakazi wa kaunti ya Kisumu wamepongeza hatua ya Rais William Ruto ya kupata ufadhili kutoka serikali ya China, kufanikisha ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Nakuru hadi Kisumu

Katika ziara yake ya siku nne nchini China, kiongozi wa taifa alifanikiwa kupata ufadhili huo mpya, ambao utapiga jeki mfumo wa serikali ya Kenya Kwanza wa kuimarisha uchumi wa taifa hili kutoka chini almaarufu Bottom-up Economic Transformation Agenda (BETA).

Utakapokamilika,  reli hiyo ya SGR itachochea ukuaji wa uchumi pamoja na kubuni fursa za uwekezaji kwa mamilioni ya Wakenya hususan Magharibi mwa nchi.

Reli hiyo ya SGR, inatarajiwa kuunganisha Kisumu na Malaba, na kuimarisha biashara kati ya Kenya na mataifa ya Afrika Mashariki.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Kisumu, Gavana wa kaunti hiyo Anyang Nyong’o, alimpongeza Rais Ruto kwa kufufua tena mradi huo ambao ulikuwa umekwama.

“Mradi huu umejadiliwa kwa muda mrefu. Tunapongeza kufufuliwa kwake, hongera kwa Rais Ruto,” alisema Gavana Nyong’o.

Utakapokamilika, reli hiyo haitachochea tu ukuaji wa uchumi katika eneo hilo, lakini pia itafanikisha utangamano wa kanda hii.

Website |  + posts
Share This Article