Mamia ya wakazi wa Butembo mashariki mwa DRC, wameandamana, kupingana maafikiano kati ya serikali yao na ile ya Rwanda kuhusu kusitishwa kwa mapigano nchini Congo.
Rai hao wanaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23, ambao wamekuwa wakichangia mapigano katika Jamhuru ya Demokrasia ya Congo.
Manandamano hayo yaliuzuka wakati Rais Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, walikuatana mjini Luanda, Angola na kusaini mwafaka wa kusitisha vita.
Waaandamanaji hao waliandamana kupinga mazungumzo ya amani baina ya Tshisekedi na Kagame.