Wagombea 7 waorodheshwa kwa wadhifa wa msajili mkuu wa mahakama

Martin Mwanje
1 Min Read

Wagombea saba wameorodheshwa na Tume ya Huduma za Mahakama, JSC kuwania wadhifa wa Msajili Mkuu wa Mahakama. 

Mahojiano ya saba hao yamepangwa kufanyika Machi, 18 mwaka huu kabla ya JSC kumchagua atakayeibuka kidedea kuwa msajili mkuu mpya wa mahakama.

Jumla ya watu 43 walituma maombi ya kutaka kumrithi Anne Amadi aliyeondoka katika wadhifa huo baada ya kukamilika kwa kipindi chake cha miaka 10 ya kuhudumu.

Saba hao walioorodheshwa ni Macharia Rose Wachuka, Ouma Jack Busalile Mwimali, Mokaya Frida Boyani na Wambeti Anne Ireri.

Wengine ni Ndemo Paul Maina, Kendagor Caroline Jepyegon na Kandet Kennedy Lenkamai.

“Kwa hivyo, inataarifiwa kwa umma kuwa mahojiano ya wagombea walioorodheshwa yatafanywa na JSC Machi 18, 2024 katika chumba cha JSC kilichopo katika jumba la CBK Pension Towers,” alisema Jaji Mkuu Martha Koome ambaye pia ni mwenyekiti wa JSC.

“Umma unaalikwa kupatiana kwa maandishi taarifa yoyote kuhusiana na wagombea walioorodheshwa.”

Tangazo la JSC kuhusiana na wadhifa huo ni kama ifuatavyo:

https://twitter.com/jsckenya/status/1758348739419296191/photo/1

 

Share This Article