Wafungwa 85 raia wa Ethiopia walio katika gereza la Illasit, kaunti ya Kajiado wakisubiri kurejeshwa nyumbani wamesusia chakula.
Wafungwa hao, wakiwemo wanaume na wanawake, walikamatwa na polisi tarehe 20 mwezi huu na kupelekwa katika mahakama ya Loitoktok iliyoamrisha kurejeshwa kwao nchini Ethiopia.
Polisi wanasema raia hao walipatikana wamefungiwa katika chumba kimoja ambacho mwenyewe hajabainika, na yamkini walikuwa katika safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta kazi.
Kulingana na polisi, watu hao walisusia chakula Februari 27 wakidai kurejeshwa kwao baada ya shughuli hiyo kucheleweshwa kwa muda.
Watoro hao wameapa kususia chakula hadi warejeshwe kwao, hatua ambayo imesababisha wao kuwa wadhaifu.
- Dismas Otukehttps://swahili.kbc.co.ke/author/dismasotuke/
- Dismas Otukehttps://swahili.kbc.co.ke/author/dismasotuke/
- Dismas Otukehttps://swahili.kbc.co.ke/author/dismasotuke/
- Dismas Otukehttps://swahili.kbc.co.ke/author/dismasotuke/