Wafugaji wa kuku wanufaika Busia

Selyne Wamala
1 Min Read

Vijana na wafugaji wa kuku katika kaunti ya Busia walipigwa jeki baada ya kukabidhiwa vifaranga 4,000, chanjo, makoo na vyakula vya kuku vilivyotolewa na Mpango wa Usaidizi wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo. 

Wakulima wa kundi la ufugaji kuku la Asiriam wakiongozwa na Celestine Okute walisema mradi huo utawaletea mapato na kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Mkurugenzi wa Mimea na Mifugo katika kaunti ya Busia Dkt. Allan Ogendo alisema kaunti hiyo ina vituo vinne vya kuangulia vyenye uwezo wa kuangua vifaranga 40,000 kila mzunguko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo Phaustine Unoi alitoa wito kwa wafugaji wa kuku kukumbatia mradi huo ili kuinua viwango vyao vya maisha.

Kauli sawia zilitolewa na Kamishna wa kaunti ya Busia Kipchumba Rutto aliyetoa wito kwa wafugaji hao kutumia sekta hiyo kufanya biashara na hivyo kujiinua kiuchumi.

 

Selyne Wamala
+ posts
Share This Article