Wafanyakazi wa afisi ya Naibu Rais aliyeng’atuliwa mamlakani Rigathi Gachagua, wameagizwa kwenda likizo ya lazima mara moja.
Kulingana na arifa iliyoandikwa na Katibu Mwandamizi Patrick Mwangi, wafanyakazi hao ni wa viwango vya T na U.
Pia wafanyakazi wa mikataba maalum wamelazimishwa kwenda likizo, huku wasimamizi wa idara mbalimbali, wakitakiwa kuapanga upya majukumu ya watakaosalia kazini.