Dhamira yetu ni kuikomboa Kenya, wasema viongozi wa upinzani

Martin Mwanje
1 Min Read

Viongozi wa upinzani sasa wanasema dhamira yao ya kuja pamoja ni kuifanya Kenya kuwa mahali salama pa kila mtu kuishi. 

Wanasema watalifikia hili kwa kuwakiliza Wakenya katika utekelezaji wa sera zao ikiwa watafanikiwa kuingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

“Bado tuna nia ya kuwashirikisha Wakenya. Pamoja, tutaangazia madhila ya kihistoria, kusahihisha makosa, na kurejesha uadilifu kwa serikali yetu,” alisema Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua.

Aliyasema hayo wakati wakiwahutubia raia katika eneo la Wamunyu, eneo bunge la Mwala katika kaunti ya Machakos.

Waliokuwapo ni pamoja na vinara Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper, Martha Karua wa PLP, Eugene Wamalwa wa DAP-K na Justin Muturi wa DP miongoni mwa viongozi wengine.

Viongozi hao walielezea imani kwamba ifikapo mwaka 2027, muungano wao utafanikiwa kuibandua serikali ya Kenya Kwanza madarakani.

 

Website |  + posts
Share This Article