Wafanyakazi wa ‘jua kali’ kunufaika na bima ya ulinzi wa jamii

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali imekusudia kuhakikisha wafanyakazi katika sekta isiyokuwa rasmi maarufu kama “jua kali” wanapewa bima ya ulinzi wa jamii chini ya Ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza ya Mabadiliko ya Kiuchumi kuanzia Chini hadi Juu. 

Waziri wa Leba Florence Bore anasema hiki ni kigezo muhimu katika kujenga mfumo wa kina, unaojitosheleza na endelevu wa kinga ya jamii kwa Wakenya wote.

Bore aliyasema hayo alipozindua Mkakati wa Uongezaji wa Bima ya Ulinzi wa Jamii kwa Wafanyakazi katika Sekta Isiyokuwa Rasmi na wanaofanya kazi katika Sehemu za Mashambani nchini Kenya.

“Hatua hii katika sekta ya ulinzi wa jamii inaashiria dhamira ya serikali katika kuhakikisha Wakenya wote wanaishi maisha mazuri na kutumia uwezo wao kama ilivyoelezwa katika katiba ya nchi,” alisema Waziri Bore wakati wa uzinduzi huo.

Ni uzinduzi uliohudhuriwa na wawakilishi kutoka Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi, COTU , FKE , ILO , NSSF , MSEA , NHIF , UNHCR na UNICEF miongoni mwa washirika wengine.

Wanane kati ya watu kumi wanaofanya kazi humu nchini wanafanya kazi katika sekta isiyokuwa rami au katika sehemu za mashambani.

Share This Article