Wabunge wa Kaskazini Mashariki wakutana kuangazia mustakabali wa eneo hilo

Martin Mwanje
1 Min Read
Faram Maalim - Mbunge wa Lagdera

Wabunge kutoka Kaskazini Mashariki mwa nchi wameandaa kongamano la siku tatu katika hoteli moja mjini Mombasa. 

Lengo la kongamano hilo ni kujadili namna ya kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazolikumba eneo hilo.

Miongoni mwa changamoto hizo ni kutengwa kwa eneo hilo, miundombinu mibovu iliyozagaa maeneo mengi, uhaba wa walimu ambao umekuwa kikwazo kwa utoaji wa masomo ya viwango vya juu na ukosefu wa usalama ambao umechangia vifo vya watu kadhaa na wengine kuwachwa wakiuguza majeraha.

“Changamoto hizi zote zimekuwa kikwazo kwa maendeleo ya eneo hili,” linasema kundi la wabunge hao likiongozwa na mbunge wa Lagdera Farah Maalim na ambalo mwenyekiti wake ni mbunge wa Garissa Mjini Adan Keynan.

Adan Keynan – Mbunge wa Garissa Mjini

Washikadau wengine wanaotarajiwa kuhudhuria kongamano hilo ni viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya eneo la Kaskazini Mashariki.

Share This Article