Waafrika hawahitaji viza kuingia Rwanda

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rwanda imeondoa hitaji la viza kwa Waafrika wote wanaoingia nchini humo. 

Hatua hiyo inaifanya Rwanda kuwa nchi ya nne barani Afrika kufanya hivyo baada ya hatua sawia kuchukuliwa na nchi za Benin, Gambia na Ushelisheli.

Tangazo la Rwanda kuondoa hitaji la viza kwa Waafrika wanaoingia nchini humo  lilitangazwa jana Alhamisi na Rais Paul Kagame.

Rais Kagame alisema, “Mwafrika yeyote anaweza kuingia nchini Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu.”

Aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kupiga jeki sekta ya utalii ya nchi hiyo.

Rais William Ruto amekuwa akishinikiza mataifa ya bara la Afrika kuwaondolea raia wa bara hilo hitaji la viza.

Tayari ametangaza kuwa Kenya itawaondolea Waafrika wote hitaji la viza kufikia mwaka 2024.

Ikiwa hilo litafanyika, basi Kenya itakuwa nchi ya tano kuchukua hatua hiyo barani Afrika.

Website |  + posts
Share This Article