Visa viwili zaidi vya Mpox vyaripotiwa hapa nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Visa viwili vipya vya Mpox vyanakiliwa hapa nchini.

Wizara ya afya imethibitisha visa viwili zaidi vya ugonjwa wa Mpox, na kufikisha 33 idadi jumla ya visa vilivyo nakiliwa hapa nchini tangu ugonjwa huo ulipozuka.

Katibu katika idara ya afya ya umma Mary Muthoni, amesema visa hivyo viwili  vimeripotiwa katika kaunti za Kericho na Taita Taveta.

Kulingana na Muthoni jumla ya watu 225 waliotangamana na waathiriwa wametambuliwa, huku 216 kati yao wakichungzwa kwa muda wa siku 21.

“Kati ya hao, watu tisa walipatikana kuwa na ugonjwa huo wa Mpox,” alisema katibu huyo.

Wakati huo huo, Muthoni alidokeza kuwa watu milioni 2.9 wamefanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo katika vituo vya mpakani, huku walioonekana na dalili za ugonjwa huo wakifanyiwa uchunguzi zaidi.

Aidha alisema kuwa sampuli za Mpox hufanyiwa uchunguzi katika maabara ya taifa ya afya ya umma (NPHL) pamoja na maabara zingine za washirika, ambapo kati ya sampuli 379 zilizofanyiwa uchunguzi, 33 zilipatikana kuwa na ugonjwa huo.

Huku muhula wa kwanza wa masomo unapoanza, katibu huyo alithibitisha kuwa wanafunzi hawako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo, akiongeza kuwa wizara ya afya kwa ushirikiano na wizara ya elimu zimeimarisha mafunzo kuhusu afya na pia zimeweka mikakati katika shule kuzuia ueneaji wa Mpox katika taasisi za elimu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *