Timu ya taifa ya Kenya kwa wanawake Harambee Starlets itashuka dimbani Félix Houphouët-BoignyBoung mjini Abidjan, Ivory Coast kwa mchuano wa kujipima nguvu dhidi ya Benin.
Kenya iliyowasili Abidjan juzi watamaliza udhia dhidi ya wenyeji Ivory Coast kwa pambano la pili la kujinoa makali Jumatano hii .
Baadaye Starlets watafunga safari kuelekea Ufaransa kwa kambi ya wiki mbili kabla ya kutua Morocco kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON).
Starlets wanaofunzwa na Beldine Odemba watafungua WAFCON kundini A dhidi ya wenyeji Morocco tarehe 17 mwezi huu.
Timu nyingine kundini humo na Kenya ni Algeria na Senegal.