Bingwa wa Olimpiki katika mita 10,000 Joshua Cheptegei wa Uganda, amejiondoa kushiriki makala ya 20, ya mashindano ya riadha duniani yatakayoandaliwa mjini Tokyo Septemba mwaka huu.
Cheptegei ambaye alinyakua dhahabu yake ya kwanza ya Olimpiki mjini Tokyo amesema lengo lake ni kushiriki mbio za barabarani za Antrim Coast Half-Marathon Agosti 24, hivyo kukosa kutetea taji ya dunia mjini Tokyo.
Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 28, atakosa mashindano ya dunia kwa mara ya kwanza baada ya kunyakua dhahabu katika makala ya mwaka 2019,mwaka 2021 na mwaka 2023.
Aidha Cheptegei ambaye ni afisa wa polisi anapanga kushiriki mbio za marathon kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba.