Baadhi ya viongozi wa makanisa na wa kisiasa katika kaunti ya Nandi wameunga mkono msimamo wa Rais William Ruto na serikali yake kuhusu maandamano ya kizazi cha “Gen Z”.
Akizungumza jana huko Nyahururu alikohudhuria ibada, Rais alisema wako tayari kufanya mazungumzo na vijana hao wa Gen z ili kuimarisha usalama na kuboresha uchumi wa Taifa hili.
Wakizungumza Kwenye hafla mbali mbali za jana Jumapili Katika eneo la Aldai na Nandi Hills, viongozi hao waliitaka huduma ya ujasusi nchini NIS Kuchunguza mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofadhili maandamano.
Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei alisema kwamba maandamano hayo yanaweza kusambaratisha mipango ya serikali na iwapo nia ya vijana hao ni njema basi watawasikiliza.
Gavana wa Nandi Stephen Sang kwa upande wake alisema tatizo kubwa la vijana ni ukosefu wa ajira na kufunguliwa kwa vituo vya kimtandao katika kila wodi nchini huenda kukatoa suluhisho kwani vijana wanaweza kupata ajira mitandaoni.
Hata hivyo wanasema watashirikiana na wabunge wote wa UDA kuhakikisha mswada wa fedha unapitishwa mapema kwa manufaa taifa.