Vijana wanaojihusisha na uhalifu Kwale waonywa

Kbc Digital
1 Min Read
Fatuma Achani - Gavana wa Kwale

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani ametoa onyo kali kwa vijana wanaojihusisha na visa vya kihalifu katika maeneo ya Denyenye, Ng’ombeni, Waa, Kombani, Tiwi na maeneo ya Diani na Ukunda akisema kuwa serikali itawakabili bila huruma.

Achani aliyekuwa akizungumza huko Ukunda katika halfa ya ugavi wa basari kwa wanafunzi wa shule za upili za kitaifa katika eneo bunge la Msambweni, amevitaka vitengo vya usalama katika ukanda wa kusini mwa Pwani kuwa macho na kuwakabili vijana wanaojihusisha na visa vya utovu wa usalama vinayohatarisha sekta ya utalii ambayo ni kitega uchumi kikuu kwa wakazi wa Diani na maeneo mengine Kwale.

Kauli iliyoungwa mkono na Naibu Kamishna wa Msambweni Josephat Mutisya aliyetaja umuhimu wa viongozi kushirikiana kukabili visa vya utovu wa usalama Diani.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *