Maelfu ya vijana wa Gen Z walifurika katika Bustani ya Uhuru katika kaunti ya Nairibi siku ya Jumapili, kuwakumbuka wenzao waliouawa wakati wa maandamano ya kitaifa wiki mbili zilizopita.
Vijana hao walisimika misalaba iliyoandikwa majina ya waliofariki katika bustani ya Uhuru Park.
Baadaye wanatarajiw akuandaa tamasha litakoongozwa na wasanii wengi akiwemo Juliani.
Hafla hiyo ilitumika kama mojawapo ya maadhimisho ya siku ya saba saba, ambayo huadhimishwa Julai 7 kila mwaka.