SGR yarejesha huduma za usafirishaji mizigo na abiria

Dismas Otuke
0 Min Read

Kampuni ya Kenya Railways imetangaza kurejesha huduma za usafirishaji mizigo kati ya Mariakani na Mombasa, baada ya kusitishwa kutokana na mvua kubwa iliyokuwa imeharibu reli katika eneo hilo.

Pia usafiri kwa kutumia treni za SGR umerejea kama kawaida baada ya kusitishwa Jumamosi iliyopita.

Kenya Railways imewahakikishia Wakenya usalama wao licha ya mvua kubwa inayoshuhudiwa katika maeneo ya Pwani.

Share This Article