Vera Sidika na Brown Mauzo waonyesha mwanao wa pili kwa mara ya kwanza

Marion Bosire
1 Min Read

Vera Sidika na aliyekuwa mume wake Brown Mauzo wamechapisha picha za mwanao wa pili kwa mara ya kwanza kabisa.

Sidika alichapisha picha akiwa amembeba mtoto huyo wa kiume kwa jina Ice Brown kwenye Instagram na kuandika kwamba Mungu alimbariki na mtoto huyo mwenye sura nzuri huku akimtakia mema anapotimiza umri wa miezi saba.

“Ninakutakia sio tu furaha na afya njema lakini pia ninaahidi kwamba nitajikakamua kuhakikisha unakua na maisha mazuri.” ndiyo baadhi ya maneno ya mama huyo wa watoto wawili.

Lakini mwisho wa chapisho hilo, Sidika alielezea kwamba alilazimika kuchapisha picha hiyo kwa sababu Brown Mauzo ambaye walitengana alitangulia kuchapisha picha ya mwanao kwa mara ya kwanza bila kumshauri.

Brown ambaye ni mwanamuziki alikuwa amechapisha picha ya Ice kwenye Instagram akimtaja kuwa Simba.

Hivi maajuzi aliporejea kutoka Marekani, Vera Sidika ambaye alilakiwa na mwanawe wa kwanza wa kike Asia alisema kwamba mwanawe wa pili hangepelekwa katika uwanja wa ndege kumlaki kwa sababu hawakuwa wametoa rasmi picha yake kwa umma.

Alipoulizwa kuhusu Brown Mauzo kwa sababu wengi wanadhania kwamba bado wako pamoja hata ingawa walitangaza utengano, Sidika alisema kwamba hamtaki kabisa karibu naye.

Share This Article