Uteuzi wa Mawaziri Wasaidizi (CASs) wasitishwa, washauri kupunguzwa kwa 50%

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto ametangaza kuwa mpango uliokusudiwa na serikali wa kuwateua Mawaziri wasaidizi, CASs umesitishwa. 

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya serikali kufuatia kukataliwa kwa Mswada wa Fedha 2024.

Hata hivyo, mpango ulikuwa umekatiliwa vikali na Wakenya waliosema uteuzi wa mawaziri wasaidizi utakuwa matumizi mabaya ya fedha za serikali wakati ambapo nchi inakumbana na changamoto za kiuchumi za kila aina.

Awali, Rais Ruto alikuwa ametangaza kuteuliwa kwa takriban mawaziri wasaidizi 50 kabla ya uteuzi huo kupigwa breki na mahakama.

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero, aliyekuwa Seneta mteule Millicent Omanga, aliyekuwa Seneta wa Kisumu Fred Outa na aliyekwa Naibu Gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wameteuliwa kwenye wadhifa huo.

Hata hivyo, Outa na Maangi ni miongoni mwa viongozi ambao baadaye waliteuliwa kwenye nafasi za kibalozi.

Wakati huohuo, Rais Ruto ametangaza kuwa idadi ya washauri serikalini itapunguzwa ndani ya utumishi wa umma mara moja.

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wakenya kuwa serikali imewaajiri washauri wengi ambao wamefanya kiasi kikubwa cha fedha kutumiwa kulipa mishahara yao.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *