Serikali imetoa hakikisho la kukamilisha usafishaji wa mto Nairobi kwa muda wa miezi 18 ijayo.
Waziri wa Mazingira Aden Duale ametangaza haya leo alipoongza sherehe za kuadhimisha siku ya kitaifa ya mazingira katika bustani ya Arboretum kaunti ya Nairobi mapema Alhamisi.
Duale amesema wametoa arifa kwa kampuni na vichinjio katika kaunti ya Nairobi kuhusu kusitisha kumwaga majitaka kwenye mto huo.
Kulingana na Waziri, usafishaji wa mto Nairobi inatakelezwa kutoka Naivasha hadi Athi River katika eneo la Z corner Juja Farm.
Mazingira Dei ilibadilishwa jina kutoka Utamaduni dei April mwaka huu, baada ya Rais Ruto kuidhinishwa sheria iliyopitishwa na bunge.
Kenya imepanda miche milioni 481 tangu Januari mwaka huu, huku serikali ikilenga kuafikia idadi ya miti bilioni 15 ifikiapo mwaka 2032.
Serikali ilianzisha mpango wa kitaifa wa upanzi wa miti kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.