Chama cha upinzani, ACT-Wazalendo, kimepinga matokeo ya uchagauzi wa urais visiwani Zanzibar baada ya Tume ya uchaguzi kumtangaza Hussein Mwinyi kama mshindi.
“Wananchi wa wameibiwa sauti yao… Suluhu pekee ya kupata haki ni uchaguzi mpya,” kilisema chama hicho.
Afisa mkuu wa chama aliiambia shirika la habari la AFP kwamba masanduku ya kupigia kura yalikuwa mengi, watu waliruhusiwa kupiga kura mara kadhaa bila kitambulisho na mawakala wao wa uchaguzi walitukuzwa kwenye vyumba vya kuhesabia kura.
Chama tawala (Chama Cha Mapinduzi: CCM) kinapanga kufanya mkutano na waandishi wa habari baadaye leo.
Wafuasi wa upinzani Zanzibar, waliionekana wakitoa malalamishi yao kwa hofu.
“Hakujawa na uchaguzi wa kuaminika tangu mwaka 1995,” alisema mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70, akiashiria kura ya kwanza ya Tanzania ya vyama vingi.
Hakuna hata mmoja wa waliohojiwa aliyetaja jina lake.
“Tunaogopa kuongea kwa sababu wanaweza kuja nyumbani kwetu na kutuchukua,” alisema mmoja.
Othman Masoud aliyegombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ACT- Wazalendo ni mwanasheria mwenye taaluma ya juu na uzoefu mpana serikalini.
Kabla ya kuingia rasmi katika siasa za upinzani, aliwahi kuwa Mkurugenzi mkuu wa mashtaka (2002–2011) na baadaye mwanasheria mkuu wa Serikali wa Zanzibar.