Ukulima wa pareto katika kaunti ya Elgeyo Marakwet uliimarika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.
Zao la pareto liliongezeka maradufu mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana huku kaunti hiyo ikilenga uzalishaji wa kilo 200,000 za pareto kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Utawala wa Gavana Wesley Rotich unadhamiria kuongeza uzalishaji wa pareto katika kaunti hiyo hadi kilo milioni moja katika kipindi cha miaka miwili ijayo na hivyo kuleta mapato ya zaidi ya shilingi milioni 300.
Rotich alisema mradi huo ni sehemu ya sera ya kuzalisha mali kwa kutumia mimea mbalimbali ya uzalishaji katika maeneo matatu ya ikolojia katika kaunti hiyo kama njia ya kupunguza ufukara asilimia 42-46 ya wakazi wa kaunti hiyo.