Ujenzi wa mitaro ya kupitisha maji katika mashamba ya Mwea kukamilishwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Ukaguzi wa ujenzi wa mitaro ya kupitisha maji. Picha/KNA

Ujenzi wa mitaro ya kupitisha maji uliokuwa umekwama katika mpango wa unyunyuziaji mashamba maji wa Mwea utakamilishwa katika muda wa miezi miwili ijayo.

Mitaro hiyo ambayo ilikuwa ya  kilomita  2.4, ilikwama baada ya kilomita 1.5 na kutatiza usambazaji wa maji katika mashamba.

Akiongea wakati wa ziara ya kujifahamisha na mashamba hayo, katibu katika idara ya unyunyuziaji maji mashamba Elphantus Kimotho alisema kukamilishwa kwa uchimbaji wa mitaro hiyo kutanufaisha zaidi ya wakulima  5,600.

“Tunatarajia kuwa wakulima wengi watapata maji baada ya kukamilishwa kwa ujenzi wa mitaro hyo. Kutokana na mbinu zilizopo za kuvuna mchele, tunatarajia kuwa hasara baada ya mavuno itapungua,”alisema Kimotho.

Alipongeza utekelezaji wa mradi huo akisema utasaidia kupunguza gharama ya uzalishaji na hasara zinazotokea baada ya mavuno.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kitaifa ya Unyunyuziaji Mashamba Maji Mhandisi Gilbert Maluki alisema halmashauri hiyo imejitolea kuhakikisha wakulima wote wanapata maji ya kunyunyuzia maji mashamba.

Website |  + posts
Share This Article