Uhispania kwenye njia panda baada ya uchaguzi mkuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Uhispania imejipata kwenye njia panda ya mrengo wa kulia na ule kushoto kushindwa kutwaa ushindi katika mchakato wa kuunda serikali mpya kufuatia uchaguzi wa Jumapili .

Chama cha upinzani cha People’s party kilizoa viti 136 vya ubunge huku chama tawala cha Waziri Mkuu Pedro Sanchez Social Worlkers Party kikipata viti 122 vya ubunge kufikia Jumapili usiku wa manane.

Idadi hiyo inaiwacha Uhispania kwenye njia panda kwani hakuna chama kilichopata viti vinavyostahili kuunda serikali .

Itabidi vyama hivyo viwili kugawana ili kuunda serikali mpya,kwani idadi ya wabunge wa upinzani licha ya kuwa wengi kuliko wale wa serikali haitoshi kumng’atua waziri mkuu  Sanchez.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *