Ufaransa iliwagusha Brazil na kuwazabua mabaoa 2-1 katika mchuano wa kundi F uliopigwa Jumamosi jioni mjini Brisbane nchini Australia.
Eugenie Le Sommer aliwaweka Ufaransa uongozini kunako dakika ya 17 na uongozi huo kudumu hadi mapumzikoni huku Brazil wakibanwa mchezoni hadi mapema kipindi cha pili ambapo Debinha kusawazisha dakika ya 58.
Nahodha Wendie Renard alipachika bao la ushindi kwa kichwa katika dakika ya 83 na kuwapa Ufaransa ushindi ambao unawachupisha kileleni pa kundi hilo kwa pointi 4 sawa na Jamaica walioifyatua Panama goli moja kwa bila nao Brazil ni wa tatu kwa alama 3 .