Ahly wamtafuta kocha mpya baada ya kumtimua Koller

Koller anaondoka timu hiyo chini ya siku 50 kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia baina vilabu nchini Marekani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara 11 wa taji ya Ligi ya mabingwa Afrika Al Ahly, wanamtafuta kocha mpya baada ya kumtimua Marcell Koller, kutoka Uswizi, baada ya miamba hao kubanduliwa katika nusu fainali ya Ligi ya mabingwa mwaka huu.

Koller anaondoka timu hiyo chini ya siku 50, kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia baina vilabu nchini Marekani.

Mswizi huyo alitwaa mikoba ya ukufunzi Septemba mwaka 2022, akiwasaidia Ahly maarufu kama Red Devils kunyakua Ligi ya mabingwa mwaka 20023 na 20024, akisimamia mechi 159, akishinda 108, sare 33 na kupoteza 17.

Hata hivyo, msimu huu Koller, amekumbwa na masaibu mengi iliweko kushindwa kwenye fainali ya kombe la CAF Super, kwa watani wao Zamalek, na pia wanakalia nafasi ya pili kwa pointi 43, alama 4 nyuma ya viongozi Pyramids.

Website |  + posts
Share This Article