Iran yajiondoa kushiriki Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Iran imetangaza kujiondoa rasmi kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa mwezi Juni hadi Julai mwaka huu na mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.

Jana Jumatano, Waziri wa Michezo wa Iran aliapa kuwa wamejiondoa baada ya Marekani kushirikiana na Israel kushambulia nchi hiyo na kumuua kiongozi wao wa kidini Ayatollah Ali Khamenei.

Iran imejumuishwa kundini G katika fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa nchini Iran kati ya Juni 11 na Julai 19 mwaka huu.

Aidha, Iran waliratibiwa kucheza mechi zote za makundi  nchini Marekani.

Share This Article