Ufaransa na Uhispania zatamba katika maandalizi ya Euro

Dismas Otuke
1 Min Read

Ufaransa na Uhispania zilitia fora katika matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya fainali za kombe la Euro kuanzia Juni 14 mwaka huu.

Ufaransa ikicheza nyumbani ilikuwa na wakati mgumu, kabla ya kuikwatua Luxembourg mjini Metz, mabao 3 kwa bila ukiwa ushindi wa nane nyumbani kati ya michuano tisa ya kujinoa makali.

Mshambulizi aliyejiunga na Real Madrid maajuzi Kylian Mbappe, alikuwa nyota wa mechi hiyo akichangia kufungwa kwa magoli mawili naye akaongeza la tatu.

Randol Kolo Muani na Jonathan Clauss walipachika magoli mengine ya Ufaransa.

Uhispania wakicheza nyumbani waliikung’uta Andora magoli matano kwa sifuri,Mikel Oyarzabal akicheka na nyavu mara nne, naye Fernando Torres akaongeza la tano .

Fainali za Kombe la Euro zitaandaliwa nchini Ujerumani kati ya Juni 14 na Julai 14.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *