Tuzo za wanawake wasanii na wanamichezo kuandaliwa mwezi ujao Tanzania.

Marion Bosire
1 Min Read

Yvonne Cherrie Khamis, ambaye ni mwigizaji nchini Tanzania na ambaye wengi wanamfahamu kama Monalisa ametangaza kwamba msimu wa pili wa tuzo za wanawake walio katika sekta ya michezo, sanaa na utamaduni utaandaliwa mwezi ujao.

Hafla ya kutoa tuzo hizo katika vitengo 30 itafanyika jijini Dar es salaam Novemba 29,2024.

Monalisa alisema kwamba mwaka huu tuzo hizo zitakuwa tofauti na za mwaka jana ambapo wawaniaji watakuwa kwa maeneo yao ya kawaida ya kazi na kufuatilia utoaji huo wa tuzo kwenye runinga.

Alitangaza pia namna ya kuafikia orodha ya wawaniaji ambapo alisema watumizi wa mitandao ndio watapendekeza majina kati ya Novemba mosi na Novemba 11, 2024.

Kurasa za mitandao za kutuma majina ya wawaniaji ni pamoja na wake binafsi @Monalisatz, @Mwafrikaasilia,@Sinema Zetu, na @AzamTV.

Shughuli ya kupiga kura itaanza Novemba 12 ikamilike Novemba 21, 2024 na kila kipengee kitakuwa na washindani wanne.

Website |  + posts
Share This Article