Timu za Tusker FC,Ulinzi Stars,Police FC na 3K iliyopandishwa ngazi msimu huu zimesajili ushindi katika mechi nne za Ligi Kuu ya Sportpesa zilizopigwa Jumatatu katika viwanja mbalimbali.
Wanajeshi Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Vapor, walijikuta taabani kunako kipindi cha kwanza baada ya Elie Asieche, kuwaweka wageni Mathare United uongozini kunako dakika ya tatu ya mchezo.
Ulinzi walirejeshwa mchezoni kwa bao la dakika ya 46 lake David Mwangi,kabla ya Leonlevit Osiago ,kuongeza la pili na la ushindi dakika ya 76.
Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Ulinzi ndani ya mechi tano.
Katika uwanja wa Afraha kaunti ya Nakuru ,bao la dakika ya 13 lkake Brian Chonjo, lilitosha kuwapa Police FC ushindi wa pili msimu huu.
Tusker FC walisajili ushindi wa 3-1, katika uga wa Sporpesa Arena kaunti ya Muranga, dhidi ya Mara Sugar nao 3K FC kutoka Embu wakainyoa Posta Rangers 2-1.