Tusker FC wanasa wanandinga watano wapya tayari kwa msimu wa ligi kuu

Dismas Otuke
2 Min Read

Tusker FC wamethibistisha kuwasajili wachezaji watano katika harakati za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya soka nchini FKF mwaka 2023 na 2024.

Wanandinga walionaswa na wagema mvinyo hao ni pamoja Joseph Mwangi, James Kibande, Fabian Adikiny, na Mganda John Byamukama, huku kipa Edwin Simiyu akipandishwa hadhi kutoka kwa timu ya chipukizi.

Mwangi, alien a umri wa miaka 26, anatua ugani Ruaraka kutoka Nzoia Sugar alikopiga soka kwa misimu minne akipachika magoli 14 na kuchangia mengine 7 katika mechi 30 alizosakata.

Kibande pia anajiunga na Tusker akitokea Nzoia Sugar FC akiwa mwanafunzi wa zamani wa shule ya St. Anthony’s High School, Kitale, mwaka 2018.

Kwa upande wake kiungo Adikiny, alien a umri wa miaka 22, anawasili Tusker kutoka Murang’a Seal, wakati mlinda lango Bymukama akianza amali yake ya soka katika timu ya Bumate FC, kabla ya kujiunga na Tooro United na kisha Express FC na hatimaye kucheza nusu ya msimu jana katika timu ya spent Gaddafi.

Wachezaji wapya wa Tusker FC  Fabien Adikiny,James Kibade,Edwin Simiyu,John Byamukama na Joseph-Mwangi wakizinduliwa  uwanjani Ruaraka

Timu hiyo pia imethibitisha kuondoka kwa wachezaji kadhaa akiwemo nahodha Humphrey Mieno, viungo Jackson Macharia na Shami Mwinyi kipa Michael Wanjala, na mabeki Kalos Kirenge na Kevin Momanyi waliogura baada ya kukamilika kwa kandarasi zao sawia na mshambulizi wa Sudan Kusini David Majak.

Charles Momanyi na mshmbaulizi wa Uganda Deogratious Ojok wameongezewa mwaka mmoja kuendelea kuwachezea Tusker, huku Momanyi akiteuliwa kiranja mpya wa timu akisaidiwa na Brian Bwire na Michael Kibwage.

Kocha wa Tusker FC Robert Matano akizungumza punde baada ya uzinduzi wa wachezaji hao ameelezea matumaini yake na sajili hao wapya akiongeza kuwa watamsaidia katika kuafukia malengo yake ya msimu moya.

Tusker FC watafungua msimu Agosti 26 dhidi ya Bandari FC .

Website |  + posts
Share This Article