Morocco itamenyana na Afrika Kusini katika fainali ya makala ya 20 ya kipute cha Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 Jumapili hii jijini Cairo,Misri.
Morocco waliwatema nje wenyeji Misri bao moja kwa bila katiak nusu fainali ya mwisho huku Afrika Kusini, wakiwagutusha mabingwa mara saba Nigeria, kwa kuwazaba pia goli lilo hilo moja kwa sifuri.
Timu hizo nne zilizocheza nusu fainali zilifuzu kuwakilisha Afrika katika fainali za Kombe la Dunia baina ya Septemba na Oktoba mwaka huu nchini Chile.