Mabingwa mara 13 wa ligi kuu ya Kenya Tusker FC watafungua msimu mpya wa mwaka 2025/2026, Ijumaa jioni katika uwanja wa Kasarani dhidi ya Kenya Commercial Bank kuanzia saa moja usiku.
Kwa mara ya kwanza mshindi wa Ligi Kuu msimu huu atapokea shilingi milioni 20 kutoka kwa wadhamini wakuu Sportpesa.
Katika mechi nyinginezo za raundi ya kwanza Jumamosi, AFC Leopards watawaalika Sofapaka katika uchanjaa wa Ulinzi kuanzia saa kumi.
Jumapili Shabana FC wataanza msimu nyumbani kwa kukabiliana na APS Bomet iliyopandishwa ngazi msimu kwa mara ya kwanza uwanjani Gusii kuanzia saa nane adhuhuri.
Timu 18 zinashiriki ligi hiyo huku Nairobi United na APS Bomet wakipandishwa ngazi kutoka ligi ya daraja ya kwanza NSL.
Mabingwa wa Ligi hiyo, Police FC, wataiwakilisha Kenya katika kombe la ligi ya mabingwa huku Nairobi United wakishiriki kombe la shirikisho.