Shule za kakamega na St.Antony zimefuzu nusu fainali ya kindumbwendumbwe cha Super 8 kinachoendelea mjini Kisumu baada ya kutwaa uongozi wa makundi .
Jumamosi Kakamega ilitoka sare ya bao moja kwa moja na Kiringari sawia na St. Antony dhidi ya Ambira.
Kwenye mechi za mwisho St. Antony waliwapiku wenyeji Kisumu magoli mawili bila jibu nao kakamega wakawalaza Highway bao moja kwa yai.
Kufuatia matokeo hayo, timu hizo zimefuzu nusu fainali ya hapo kesho jumapili usubuhi. Kakamega itamenyana na wenzao wa magharibi Bukembe wakati St. Antony ikitesa nyasi dhidi ya Ringa kutoka eneo la Nyanza alafu washindi wakabane koo jioni katika fainali.