Tume ya huHuma za Mahakama yatangaza nafasi za kazi 221

Nafasi 20 za kazi ni za majopo huku 201 zikiwa za ajira ya muda mfupi kwa wanafunzi.

Dismas Otuke
1 Min Read
Tume ya Huduma za Mahakama.

Tume ya Huduma za Mahakama nchini (JSC) imetangaza nafasi za ajira 221 katika majopo ya kutatua migogoro nchini pamoja na mpango wa ajira ya muda mfupi kwa wanafunzi.

Kupitia kwa tangazo lililochapishwa Julai 23, JSC imewataka Wakenya walio na nia kutuma maombi kufikia Agosti 13.

Nafasi 20 za kazi ni za majopo huku 201 zikiwa za ajira ya muda mfupi kwa wanafunzi.

Baadhi ya nafasi zilizotangazwa ni ile ya Mwenyekiti wa Jopo la Kutatua Migogoro Michezoni (SDT), na pia nyingine moja katika jopo hilo isiyokuwa ya uwakili.

Aidha, JSC imetangaza nafasi ya ajira kwa Naibu Mwenyekiti wa Jopo la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Ushirika, na Mwenyekiti wa Jopo la Masoko ya Mtaji yaani Capital Markets.

TAGGED:
Share This Article