Saba wathibitishwa kufariki ajali ya helikopta Samburu

Mamlaka zinaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo iliyotokea katika vilima vya Sapache karibu na Mlima Ololokwe huko Samburu Mashariki.

Martin Mwanje
1 Min Read

Watu 7 wamethibitishwa kufariki akiwemo rubani baada ya helikopta kuanguka katika vilima vya Sapache karibu na Mlima Ololokwe huko Samburu Mashariki.

Kulingana na uchunguzi wa awali, helikopta hiyo aina ya Lady Lorry, ilikuwa ikitoka Suyian, Laikipia ikielekea Hifadhi ya Loisaba ilipoanguka majira ya saa 3:13 asubuhi leo Jumatano.

Saba waliofariki ni Josh Outran ambaye alikuwa rubani, Roger Duarte, Adam Navaty na Stephen Vascanknez.

Wengine ni Henry Parra, Michael Contugi na Suian Suarez.

Helikopta hiyo iliyoshika moto iliharibika mno.

Maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu ni miongoni mwa waliofika eneo la ajali kusaidia katika jitihada za uokozi.

Mamlaka zinachunguza chanzo cha ajali hiyo.

Share This Article