Aliyekuwa Waziri Raphael Tuju amepelekwa katika kituo cha Polisi mtaani Karen Jumatatu alasiri na kuandikisha taarifa kuhusu madai ya kutoweka kwakwe.
Tuju alinukuliwa akisema kuwa alilazimika kwenda mafichoni kwa kuhofia maisha yake na kuwakwepa watu waliokuwa wakimfuata na gari ambalo halikuwa na nambari za usajili.
Mbunge huyo wa zamani wa Rarieda pamoja na mlinzi wake Steve Mwanga, waliripotiwa kutoweka Jumamosi iliyopita huku maafisa wa polisi wakipata gari lake likiwa limeegeshwa huku milango ikiwa wazi mtaani Karen.
Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI Mohamed Amin amefichua kuwa Tuju alikuwa nyumbani kwake wakati familia yake iliripoti kutoweka kwake.