Tubi Mohamed Tubi achaguliwa mbunge wa Isiolo Kusini

Tom Mathinji
1 Min Read

Tubi Mohamed Tubi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA), ametangazwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Isiolo Kusini.

Tubi alipata kura 7,352 na kumshinda mpinzani wake wa karibu ambaye pia ni dadake Bina Tubi wa chama cha Jubilee, ambaye alipata kura 634.

Wawili hao ni wanawe mbunge wa zamani wa eneo hilo Mohamed Tubi Bidu aliyefariki mwezi Novemba mwaka jana na kupisha uchaguzi huo.

Mgombea wa chama cha National Economic Development Party, Isack Fayo, alimaliza wa tatu akiwa na kura 44.

Hii ni licha ya kujiondoa kwenye uchaguzi huo uliofanywa jana Alhamisi dakika za mwisho na kutangaza kumuunga mkono mgombea wa UDA.

Matokeo hayo yalivutia umakini mkubwa kutokana na ushindani usio wa kawaida wa ndugu wawili na mabadiliko ya hali ya kisiasa katika eneo hilo.

Hii ni mara ya pili kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inayoongozwa na Erastus Ethekon kusimamia uchaguzi tangu ilipoingia madarakani mwaka jana.

Share This Article