Trump aongoza viongozi wengine kusaini makubaliano ya kusitisha vita Gaza

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais Donald Trump baada ya kutia saini makubaliano ya amani nchini Misri / Picha kwa hisani ya abc7NY

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini waraka wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. 

Trump alitia saini waraka huo wakati wa mkutano wa viongozi wakuu ulioandaliwa jana Jumatatu katika mji wa Sharm el-Sheikh nchini Misri.

Waraka huo pia ulisainiwa na Marais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri na Recep Tayyip Erdogan wa Uturi.

Mwingine aliyeutia saini ni Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani.

Viongozi hao watatu walisimamia mazungumzo kati ya Israel na Hamas.

Viongozi kutoka zaidi ya nchi 20 walihudhuria mkutano huo.

Nao ulifanyika siku ambayo mateka 20 walioshikiliwa na Hamas waliachiliwa huru kutoka Gaza.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hakuhudhuria mkutano huo kutoka na kile alichokisema ulifanyika wakati wa sikukuu ya Wayahudi.

Aidha, kundi la Kiislamu la Hamas halikualikwa mkutanoni.

Website |  + posts
Share This Article