Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo la kuiwekea vikwazo Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), akisema mahakama hiyo inatekeleza vitendo vinavyokiuka sheria.
Kulingana na Trump, mahakama hiyo inalenga Marekani na mshirika wake wa karibu Israel.
Hayo yanajiri muda mfupi baada ya Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kushiriki mazungumzo jijini Washington, Marekani.
Mnamo mwaka 2024, ICC ilitoa agizo la kukamatwa kwa Netanyahu kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa kivita katika eneo la Gaza.
Marekani imeiwekea ICC vikwazo vya kifedha pamoja na viza ya kusafiri wachunguzi wa mahakama hiyo pamoja na familia zao.
Hata hivyo, Marekani si mwanachama wa ICC na mara kwa mara imekataa mamlaka yoyote ya chombo hicho kuhusu maafisa au raia wa Marekani.