Ruto: Marekani kuendelea kufadhili operesheni ya kiusalama Haiti

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto ametangaza kuwa operesheni ya kuleta usalama nchini Haiti inayoongozwa na Kenya, itaendelea kupokea ufadhili wa kifedha kutoka kwa serikali ya Marekani.

Tangazo hilo linajiri huku wasiwasi ukitanda kuhusu hatima ya operesheni hiyo, kufuatia hatua ya utawala wa Trump kusitisha ufadhili wa kifedha  kwa miradi kadhaa.

Rais Ruto alithibitisha kuwa operesheni hiyo ya kiusalama, haitaathiriwa na usitishaji wa ufadhili huo.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo alipozungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio.

Ruto alielezea kujitolea kwa Washington kuunga mkono mchakato wa kuleta amani nchini Haiti.

“Mazungumzo yetu yalithibitisha kuwa Marekani itafadhili mchakato wa kuleta amani nchini Haiti (MSS), kwa kutambua umuhimu mkubwa wa operesheni hiyo na jukumu lake la kuleta uthabiti na kudumisha amani,” alisema Rais Ruto.

“Tuliangazia uhusiano baina ya Kenya na Marekani na kurejelea kujitolea kwetu kuimarisha ushirikiano uliopo,” aliongeza Rais Ruto.

Aidha, Rais Ruto alidokeza kuwa hali ya usalama katika kanda hii na bara Afrika, hususan hali ilivyo katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilijadiliwa katika mazungumzo baina yao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *